Mkude ana kazi kurejea kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Oct 2023
Mkude ana kazi kurejea kikosi cha kwanza

Kiungo wa Yanga Jonas Mkude ana kazi ya kuendelea kupambana katika kiwanja cha mazoezi ili amshawishi Kocha Miguel Gamondi kumtumia kwenye kikosi chake

Mkude alianza vyema msimu akionyesha kiwango bora kilichompa nafasi ya kuitwa timu ya Taifa lakini baada ya kuchelewa kurejea kikosini kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa, akakumbana na adhabu

Hata hivyo kwa sasa amerejea akiwa sehemu ya kikosi kinachojiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Ijumaa, Oktoba 27

Gamondi aliwahi kusema katika kikosi chake kila mchezaji anayo nafasi ya kucheza jambo muhimu ni kuonyesha katika kiwanja cha mazoezi kuwa anastahili kupewa nafasi hiyo

"Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza ndani ya kikosi changu, ninachoangalia ni bidii yao mazoezini, kwani lengo ni timu kufanikiwa kwenye malengo yake," yalikuwa maneno ya Gamondi katika moja ya mahojiano yake

Katika eneo la kiungo, Mkude anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Khalid Aucho na Mudathir Yahya ambao wamejihakikishia nafasi ya kuanza

Lakini pia wapo Zawadi Mauya, Salum Abubakar na hata Pacome Zouzoua ambaye amekuwa akitumika katika maeneo tofauti kulingana na mahitaji ya mchezo

Katika mechi za karibuni Mkude hajafanikiwa kuingia hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba na hivyo ni wazi anapaswa kuendelea kupambana kwenye kiwanja cha mazoezi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’