Tangu aondoke Yanga kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' amekutana na waajiri wake hao wa zamani mara mbili na amekumbana na vipigo
Matokeo ya mechi hizo mbili pasipo na shaka yamemkumbusha Feisal ukubwa wa klabu ya Yanga na haikuwa sahihi kwake kujaribu kushindana na taasisi hiyo kubwa zaidi ya soka nchini
Jana Feisal alikumbana na zomea zomea ya mashabiki wa Yanga ambao ni kama wanajibu mapigo kutokana kile kilichotokea wakati wa mchakato wa kuondoka kwake
Wale wanaolaumu mashabiki kuwa hawakuwa sahihi kumzomea Feisal nafikiri hawafahamu vyema jukumu la shabiki ni nini awapo uwanjani
Ni hivi, kwa shabiki upenzi wa timu ndio kipaumbele cha kwanza kabla ya hayo mengine. Pale wanapoingia uwanjani majukumu yao ni mawili tu, kushangilia na kuzomea
Kushangilia ili kuiongezea hamasa timu yao na kuzomea ili kuwavuruga wapinzani wao. Ingekuwa ajabu kama mashabiki wa Yanga wangemshangilia Feisal kila alipogusa mpira, kwani hilo sio jukumu lao
Kwa upande mwingine jana pengine Feisal alionyesha kuanza kurejea katika ubora wake, kwani alikuwa na kiwango bora sana
Tafsiri ya picha hapo juu inaweza kukupa majibu mengi juu alichokuwa akifikiria Feisal
Hili linaweza kuwa somo zuri kwa wachezaji wengine kuwa ni makosa makubwa kuondoka kwa dharau katika timu iliyokupa mafanikio kwani huijui kesho yako