Stephane Aziz Ki jana alifunga hat-trik yake ya pili katika ligi kuu ya NBC tangu alipojiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga
Hat-trik yake ya kwanza aliifunga msimu uliopita uwanja wa Azam Complex katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Ni mara chache sana hat-trik hufungwa kwenye mechi za derby, na zinapofungwa zinakuwa na thamani kubwa
Ndicho kilichotokea jana uwanja wa Benjamin Mkapa, ushindi wa mabao 3-2 waliopata Yanga dhidi ya Azam Fc umewarejesha Wananchi kileleni mwa msimamo wa ligi
Katika mchezo huo Ki alimpa wakati mgumu mlinda lango wa Azam Fc, alipiga mashuti matano yaliyolenga lango huku matatu yakijaa kambani
Mabao yake sita msimu huu yanamfanya awe kinara katika mbio za ufungaji bora akimzidi bao moja mshambuliaji wa Simba Jean Baleke
Baada ya kukabidhiwa mpira, Ki aliutoa zawadi kwa Waziri wa Madini, Mh. Antony Mavunde