Gamondi asuka mkakati wa ushindi dhidi ya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2023
Gamondi asuka mkakati wa ushindi dhidi ya Azam Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anakiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili, Oktoba 22 katika uwanja wa Azam Complex

Gamondi amesema baada ya mechi tano za ligi kuu, sasa anafahamu hakuna mchezo mwepesi kwa Yanga kwa sababu kila timu inatamani kupata ushindi dhidi ya Yanga

"Nafahamu mchezo hautakuwa mwepesi hivyo tunapaswa kufanya maandalizi bora ili kuhakikisha tunakuwa katika kiwango bora cha ushindani"

"Kila timu inatamani kupata ushindi dhidi ya Yanga, mchezo dhidi ya Azam Fc hautakuwa tofauti"

"Nafahamu tulicheza nao Tanga kwenye Ngao ya Jamii tukapata ushindi wa mabao 2-0. Nakumbuka katika mchezo ule kipindi cha kwanza hakikuwa rahisi lakini tulikuwa bora sana kwenye kipindi cha pili na tukaweza kushinda"

"Nafikiri utakuwa mchezo mzuri kwa kila timu na mashabiki watapata burudani kwani naamini tutakuwa na nafasi ya kucheza mpira zaidi kuliko baadhi ya mechi tulizocheza karibuni," alisema Gamondi

Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi Avic Town kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kuhakikisha wanarudi kileleni mwa msimamo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’