Viungo washambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki wameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani kutokana na ubora wao uwanjani
Wachezaji hao ndio vinara wa kuzifumania nyavu kwenye kikosi cha Yanga katika ligi kuu ya NBC kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu
Pacome, Aziz Ki na Maxi jana walifunga mabao ya Yanga katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Geita Gold mkoani Mwanza

Maxi ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi kwani pamoja na mabao yake matatu, pia ametoa pasi tatu za mabao
Pacome ana pasi mbili za mabao wakati Aziz Ki nae ana pasi moja ya bao
Mlinzi wa kulia Yao Yao nae ametoa pasi tatu za mabao huku akiwa amefunga bao moja
Kuna watu walidhani baada ya Yanga kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc basi makali yameisha lakihi kipigo walichokutana nacho Geita Gold jana kimewakumbusha wengine kuwa bado wataendelea kuteseka sana