Lagrouni alivyomfunika Helmey Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2023
Lagrouni alivyomfunika Helmey Yanga

Msimu wa 2022/23 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga ambapo mabingwa hao wa Tanzania Bara walitwaa mataji yote ya ndani pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC)

Ilikuwa ngumu mashabiki kuamini pale walipopewa taarifa kuwa kocha wao mkuu Nasreddine Nabi anaondoka pamoja na watu wake muhimu katika benchi la ufundi

Kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akatangaza ujio wa Miguel Gamondi raia wa Argentina

Wananchi wakapewa taarifa kuwa Gamondi ataunda benchi lake la ufundi wakati huo Wananchi wakitamani kumuona tena kikosini aliyekuwa kocha wa fitnes, Helmy Gueldich

Kinyume na matarajio ya wengi, Gamondi akamtangaza, Taibi Lagrouni kutoka Morocco kuwa kocha mpya wa viungo

Lagrouni amehitaji miezi miwili tu kuwasahaulisha Wananchi jina la Helmey ambaye alijiunga na Orlando Pirates ya Afrika Kusini

Lagrouni ndiye mwenye jukumu la kuweka utimamu wa wachezaji sawa na kwa hakika ameifanya kazi yake vyema

Yanga inacheza soka gumu ambalo limewapa shida timu zote zilizokutana nazo msimu huu kukiwa hakuna timu iliyofanikiwa kuinyanyasa kwa umiliki wa mpira kwenye michezo yao 9 waliyocheza kwenye mashindano yote.

Gamondi amesema haikuwa bahati mbaya kumleta Lagrouni ambaye amewahi kuitumikia RS Berkane. Alimfahamu kwa muda mrefu

"Namjua kwa muda mrefu ni kocha mzuri mwenye uzoefu mkubwa wa kuwandaa wachezaji, kwangu mimi ni mmoja kati ya msaidizi wangu ambaye amesaidia kuwaimarisha wachezaji wetu hapa,"alisema Gamondi

Katika kuimarisha kazi ya Lagrouni mabosi wa Yanga nao wakashusha vifaa kibao vya mazoezi kambini Jijini Dar es Salaam ambavyo ni mahitaji ya kocha huyo raia wa Morocco.

Vifaa hivyo vya kumpimia kasi ya mchezaji jinsi gani amekimbia ndani ya uwanja lakini pia vifaa vya kufanyia mazoezi tofauti vimeshushwa kambi ya Yanga ambavyo vilihitajika na makocha hao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’