Matchday : Ihefu Fc vs Yanga, NBC PL, Oct 04

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2023
Matchday : Ihefu Fc vs Yanga, NBC PL, Oct 04

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako mkoani Mbeya kuwakabili Ihefu Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Highland Estates, huko Mbarali

Ni wazi hautakuwa mchezo rahisi kutokana na kile kilichotokea msimu uliopita ambapo Yanga ilipoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 katika uwanja huo wa Highland Estates

Yanga itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na lengo la kulipa kisasi kwa kuibuka na ushindi na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ambao Azam Fc wanaongoza baada ya kufikisha alama 10 jana wakilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Dodoma Jiji

Kuonyesha kuwa Yanga inautaka mchezo huo, Wananchi walitua Mbarali jana na jioni kukamilisha maandalizi yao kwenye uwanja wa Highland Estates

Msimu uliopita Yanga iliweka kambi Mbeya mjini na kuelekea Mbarali siku ya mchezo, Meneja wa Yanga Walter Harrison akidokeza kuwa uamuzi huo uliwaathiri

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi huenda leo akafanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merriikh

Baada ya mchezo wa leo, Yanga inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu katika kipindi cha siku tatu zijazo dhidi ya Geita Gold

Mchezo utapigwa kuanzia saa 10 jioni....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’