Kikosi cha Yanga tayari kiko Mbarali ambapo jioni ya leo watakamilisha mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja Highpland Estates
Tofauti na msimu uliopita, Yanga imewahi Mbarali mapema ili kuhakikisha wachezaji wanafanya mazoezi katika uwanja wa Highland Estates na kupata muda wa kuzoea hali ya hewa
Msimu uliopita hali ya hewa ilikuwa changamoto kwa wachezaji wa Yanga, kwa kiasi kikubwa ilichangia Yanga kutocheza vizuri hasa kwenye kipindi cha pili
Yanga ilichelewa kuwasili Mbeya na hivyo kwenda Mbarali siku ya mchezo huko wakakutana na kisichotarajiwa







ADVERTISE HERE