Tumerejesha heshima ya Yanga CAF CL - Mwamnyeto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2023
Tumerejesha heshima ya Yanga CAF CL - Mwamnyeto

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kitendo cha timu hiyo kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupita miaka 25, imemfanya aingie kwenye historia ya klabu hiyo akisema ndoto zimetimia kwani kila mchezaji alikuwa anaumizwa na kelele za kushindwa kutinga hatua hiyo

Yanga ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam juzi iliifunga Al Merrikh ya Sudan na kuitoa kwa jumla ya mabao 3-0, kwani mchezo wa kwanza wa ugenini timu hiyo ilishinda mabao 2-0 jijini Kigali, Rwanda na kutinga makundi tangu ilipofuzu mara ya mwisho mwaka 1998

Kitendo cha kuwepo kwenye kikosi klilichozima mzimu ulioisumbua klabu hiyo, Mwamnyeto alisema amefurahi kwa kutimiza ndoto na kuwapa raha mashabiki wa Yanga na kwamba kwa sasa wanaenda kujipanga ili kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita walipofika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika

"Nimefurahi sana kila mchezaji katika mchezo alikuwa na hamu ya kuona timu inasonga mbele na kwa jitihada na uwezo wa Mungu tumefanikiwa"

"Huko tunakoenda ndio kugumu zaidi, ila tutapambana tutafika mbali na kuiwakilisha nchi vizuri maana ni jukumu letu kama wachezaji kupambana kupata matokeo, hatua ya makundi sio mchezo maana timu zote zinakuwa bora"

"Tulivyoteleza mwaka jana viongozi waliona upungufu uko wapi na sisi wachezaji tulipambana tukashindwa kufikia hatua hii Ligi ya Mabingwa msimu huu tukakubaliana tupambane kweli kweli na Mungu kasikia dua zetu," alisema Mwamnyeto

Droo ya hatua ya makundi itafanyika Ijumaa Oktoba 06 huko Afrika Kusini ambapo kutakuwa na takribani wiki sita za maandalizi kabla ya mechi za makundi kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa Novemba 2023

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’