Hiyo Yanga mpaka kocha wa Al Merrikh kaikubali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2023
Hiyo Yanga mpaka kocha wa Al Merrikh kaikubali

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefanya kazi nzuri mpaka sasa tangu alipojiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwanzoni mwa msimu

Chini ya Gamondi Yanga haijapoteza mchezo wowote juzi akifanikiwa kuwapeleka Wananchi hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kusubiri kwa takribani miaka 25

Yanga imetinga makundi kibabe kwa ushindi wa nyumbani na ugenini dhidi ya timu ngumu ya Al Merrikh ambayo katika misimu sita iliyopita ilijihakikishia nafasi yake kwenye makundi

Haishangazi kuona Kocha wa Al Merrikh Osama Nabieh akikiri amekutana na tmu bora ambayo imempa radha tofauti ya soka la Afrika alilozoea

Nabieh alitoa maoni yake baada ya mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa Azam Complex na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, ushindi uliwapeleka Wananchi makundi kwa faida ya mabao 3-0 baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza

"Yanga wanacheza soka bora kama vilabu vikubwa barani Ulaya. Wanaonana vyema na kushambulia kwa kasi pia wakipoteza kila mmoja anautafuta mpira"

"Tumecheza na timu kubwa Afrika lakini mechi zote mbili na Yanga zimeonesha ubora wao wa hali ya juu. Sitashangaa wakiwa mabingwa Afrika msimu huu, " alisema Nabieh

Sio mara ya kwanza kwa watu kutoka nje ya Tanzania kutoa maoni kuhusu ubora wa Yanga lakini maoni hayo hapa nchini huchukuliwa kama mzawa

Msimu uliopita kila Yanga ilipopiga hatua kwenye kombe la Shirikisho ilitafutwa sababu ya kuonyesha kuwa mafanikio waliyopata sio kwa ubora wao bali kucheza na timu dhaifu

Hata msimu huu kauli hizo zilianza kusikika mapema tu walipopangwa na Asas Fc na hata walipocheza na Al Merrikh wapo waliobeza ushindi huo wakisahau kuwa hawa Al Merrikh karibu kila msimu wanacheza hatua ya makundi

Huu unaweza kuwa msimu mzuri kwa Yanga kudhihirisha ubora wake katika michuano hii ya ligi ya mabingwa kwani naamini Wananchi watakuwa na nafasi ya kukutana na timu zinazoitwa vigogo wa soka barani Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’