Hatimaye ile siku muhimu kwa Wananchi imewadia! Ni mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabinbwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh
Leo Yanga inahitaji matokeo ya aina mbili tu ili kutinga hatua ya makundi, ushindi au sare ya aina yoyote
Nje ya uwanja, ni siku itakayopambwa na shamrashamra kutoka kwa Wananchi, siku hii ikipewa jina la Aziz Ki Day
Ndio! kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki amebeba hamasa kuelekea mchezo huo
Wananchi mamia kwa mamia wanatarajiwa kuelekea uwanja wa Azam Complex wakiwa na funguo zao huku wengine wakivaa 'vinjunga' kama sehemu ya hamasa
Hadi kufikia jana asilimia 95 ya tiketi zote zilikuwa zimeuzwa, ni wazi Azam Complex itafurika Wananchi ambao wanakwenda kuishangilia timu yao ili kuhakikisha inatinga makundi baada ya kusubiri kwa takribani miaka 25
Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1 usiku..