Tumejipanga kutinga makundi - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2023
Tumejipanga kutinga makundi - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema hawana wasiwasi wowote kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merrikh utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam

Majira ya saa 1 usiku pale viunga vya Chamazi, Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Merrikh katika mchezo ambao dakika 90 zinaweza kurejesha furaha ya Wananchi wakiishuhudia tena timu yao ikicheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya kusubiri kwa takribani miaka 25

Ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga walipata ugenini katika Uwanja wa Kigali Pele, Nyamirambo nchini Rwanda, unawapa Wananchi matumaini makubwa ya kutinga hatua ya makundi 

Arafat amesema wanafahamu mchezo huo wa pili hautakuwa mwepesi lakini wana imani na kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi pamoja na wachezaji wanaounda kikosi bora cha Yanga msimu huu

"Tunajua mchezo haujamalizika, dakika 90 za mchezo wa kwanza zilikwisha pale Kigali, Rwanda na Mungu akatujaalia tukapata ushindi wa mabao 2-0 ugenini, lakini kwa kuiangalia timu yetu, maandalizi ya mwalimu Miguel Gamondi, na ubora wa kikosi chetu, basi ni matumaini yetu kuwa tunakwenda kukamilisha pale palipobakia na kusonga hatua inayofuata ya makundi"

"Kwa sasa lengo letu ambalo ni shauku ya kila Mwanayanga ni kufuzu  makundi na tukishafika huko tutajipanga ili kuona tunafika mbali kwenye michuano hiyo," alisema Arafat

Al Merrikh tayari wako nchini tangu siku ya Jumatano kocha wao akiweka wazi kuwa wamekuja kupambana kusaka ushindi na kutinga hatua ya makundi licha ya kuwa wako nyuma kwa mabao 2-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’