Uzoefu utatubeba Rwanda - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Sep 2023
Uzoefu utatubeba Rwanda - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anaamini uzoefu ambao wachezaji wa Yanga waliupata kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita, utakuwa muhimu katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh

Jumamosi Septemba 16 Yanga itakuwa Rwanda kumenyana na Al Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa uwanja wa Pele, Kigali

Msimu uliopita Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho ikikosa ubingwa kwa mujibu wa kanuni licha ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger katika mechi mbili za fainali

Zaidi ya robo tatu ya wachezaji walioipa Yanga mafanikio msimu uliopita bado wapo, Gamondi anaamini nyota hao pamoja na wengine waliosajiliwa wanafahamu nini wanapaswa kufanya

"Tuna bahati kuwa na wachezaji ambao mbali na ubora walionao na pia ni wazoefu wa michuano ya CAF, hilo halina shaka kwa namna wanavyoutamani mchezo wa El Merreikh"

"Tayari nimetoa maelekezo Kwa wachezaji wote kuhusu mambo ya kufanya ndani ya uwanja, hivyo kazi imebaki kwao kwenda kupambana ili washinde ugenini"

"Al Merreikh sio wepesi na hatujaichukulia Kwa dharau tunajua tunaenda kushindana na timu ambayo pia inahitaji nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hii, nasi pia tunaenda kushindana ili kuweza kufikia lengo ndio maana nasema tutajuana huko huko kabla ya kurudiana hapa nyumbani," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’