Yanga yajaza mabasi saba safari ya Rwanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2023
Yanga yajaza mabasi saba safari ya Rwanda

Wananchi hawana jambo dogo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki na Wanachama wa Yanga kuendelea kujiandikisha kwa ajili ya safari ya Rwanda kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh

Mpaka sasa, Yanga imethibitisha kuwa mabasi saba yamejaa baada ya mashabiki na Wanachama kulipia gharama ya safari

Kutakuwa na mabasi maalum kutoka jijini Dar es salaam ambayo gharama ni Tsh 150,000/- kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tiketi ya kuingia dimba la Pele, Kigali Jumamosi Septemba 16 2023

Pia kutakuwa na mabasi kutoka mikoa ya Kigoma, Kagera na Mwanza ambapo utaratibu unaandaliwa katika Matawi ya mikoa husika

Uwanja wa Pele unachukua takribani mashabiki 22,000, Wananchi wamepania kwenda kuujaza uwanja huo

Hapo bado hujazungumzia Wananchi wa Rwanda ambao wanaisubiri kwa hamu kubwa Yanga

Safari itakuwa Alhamisi Septemba 14, bado mashabiki wanaendelea kujitokeza ambapo zoezi litafungwa Jumanne ijayo, Septemba 12

Kwa hakika huko Rwanda Yanga itakuwa kama nyumbani tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’