Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ni nafasi nzuri kwa kikosi chake kucheza mechi ya mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya El Merrikh huko Rwanda
Septemba 16 2023, Yanga itakuwa Pele, Kigali Stadium kuumana na wenyeji wao El Merrikh ambao walichagua kutumia uwanja huo kutokana na machafuko yanaendelea nchini mwao Sudan
Gamondi amesema wana muda mzuri wa kujiandaa hapa hapa Tanzania na kusafiri kuelea Rwanda siku chache kabla ya mchezo kwani safari yao itakuwa ya saa chache na haitawasababishia wachezaji uchovu
Aidha kucheza mchezo huo ugenini lakini wakiwa na mashabiki wengi ni faida nyingine kwao
"Kucheza Rwanda nafikiri haitakuwa ratiba mbaya kwetu, tunaweza kufanya mazoezi hapa kisha tukatumia saa chache kwenda Rwanda, hiyo ni faida kubwa kwetu kwa sababu wachezaji hawatapata uchovu"
"Lakini muhimu zaidi tuna faida nyingine ambayo ni kubwa, mashabiki wetu wataweza kusafiri kutupa sapoti katika mchezo huo," alisema Gamondi
Tayari Yanga imetangaza utaratibu wa mashabiki wanaotaka kusafiri na timu kutoka jijini Dar es salaam kulipa Tsh 150,000/-
Utaratibu pia umeandaliwa kwa mashabiki wa mikoa jirani karibu na Rwanda kama Kigoma, Kagera, Mwanza ambapo gharama ni kati ya Tsh 55,000/- hadi Tsh 90,000/- kwa safari ya kwenda na kurudi Rwanda
Wananchi wa Rwanda pia wengi watakuwa na shauku ya kuishuhudia Yanga