Sasa ni zamu ya Skudu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2023
Sasa ni zamu ya Skudu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Skudu Makudubela amepona majeraha akiwa sehemu ya silaha zinazoandaliwa kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya El Merrikh

Kikosi cha Yanga kitasafiri Rwanda kuikabili El Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaofanyika uwanja wa Pele, Septemba 16

Skudu alipata majeraha katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc, akicheza kwa dakika saba tu katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Baadae hakuonekana tena uwanjani akiuguza majeraha hayo lakini sasa amepona na kurejea rasmi kikosini

Mashabiki wa Yanga tayari wameona ubora wa nyota wote waliosajiliwa isipokuwa Skudu tu, ambaye pengine wanaweza kumshuhudia nchini Rwanda

Kabla ya kupata majeraha Skudu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha kocha Miguel Gamondi

Alitumika kwa dakika 45 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs na pia kucheza mechi kadhaa za kirafiki Avic Town

Baada ya kuyaona makali ya Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua 'profesa', bila shaka ni zamu ya Skudu kuonyesha alichowaletea Wananchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’