Morali ya wachezaji Yanga iko juu

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
21 Jul 2017
Morali ya wachezaji Yanga iko juu
Kwa wiki mbili sasa kikosi cha Yanga kimekuwa kikijifua kwa nguvu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Simba Agosti 23 sambamba na ligi.

Morali ya vijana iko juu sana na wanafurahia mazoezi wanayopewa na kocha George Lwandamina licha ya kukiri mazoezi ya Mwalimu ni 'makali'.

Nahodha Nadir Haroub amesema mazoezi hayo yatawaimarisha sana na ametabiri kuwa msimu huu Yanga itakuwa moto wa luotea mbali.

Mmoja wa wachezaji alitania kuwa maandalizi yanayofanywa na Yanga yamepeleka taharuki kwa wapinzani na kujikuta wanasajili kila mchezaji mwenye jina kubwa kwa kudhani atawasaidia.

Simba imesajili karibu wachezaji wote walio kwenye kikosi cha Stars kwani imesajili wachezaji wanne kutoka klabu ya Azam ambao pia wamo kwenye kikosi cha Taifa STars.

Pia imemsajili Salim Bonde kutoka Mtibwa Sugar ambaye yumo kwenye kikosi cha Stars hivyo kupelekea baadhi ya mashabiki kukipachika kikosi hicho kinachonolewa na Salum Mayanga jina la 'Simba Stars.'

Kamati ya usajili ya Yanga imeangalia mbali zaidi kwa kusajili wachezaji ambao umri wao bado ni mdogo watakaoweza kuisaidia Yanga kwa muda mrefu.

Usajili wa Youthe Rostand, Ibrahim Ajib, Ramadhani Kabwili, Pius Buswita, Baruani Yahya na Abdallah Shaibu umeongeza chachu kwenye kikosi cha Lwandamina.

Vijana hawa wanatabiliwa kuja kuisaidia Yanga kwenye michuano mbalimbali kwani umri wao bado ni mdogo na damu inachemka.

Huwezi kufananisha na huko upande wa pili ambako wameongeza wastani wa umri wa kikosi chao!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’