Gamondi aongeza makali safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2023
Gamondi aongeza makali safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefanya kazi katika viwanja vya mazoezi kuhakikisha eneo la ushambuliaji linatumia vyema nafasi zinazotengenezwa

Yanga ilikuwa timu bora katika michuano ya Ngao ya Jamii iliyofanyika wiki iliyopita mkoani Tanga, lakini Wananchi walishindwa kutetea Ngao hiyo baada ya kushindwa kufunga bao katika dakika 90 za mchezo wa fainali dhidi ya Simba na kupoteza kwenye mikwaju ya penati

Yanga ilitawala mchezo huo wa fainali lakini lilikosekana bao la kuwahakikishia Wananchi kushinda Ngao hiyo

Baada ya kurejea Dar es salaam, kabla ya kuanza maandalizi ya mchezo wa awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc, Gamondi alifanya kikao na washambuliaji wake

Mtihani wa kwanza kwa washambuliaji Hafiz Konkoni, Kennedy Musonda na Clement Mzize ni Jumapili katika mchezo dhidi ya Asas Fc

Hesabu za Gamondi ni kuona washambuliaji wanakuwa watulivu na kutumia nafasi kufunga mabao

"Tunacheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi, ila bado tunapoteza utulivu kidogo kumalizia kule mbele, ni jambo zuri tumeliona hili mapema, hivyo tunalifanyia kazi"

"Tunahitaji kuboresha kitu na hili sio la mtu mmoja ni kati ya makocha na washambuliaji, tunaamini kutakuwa na mabadiliko taratibu," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’