Pongezi kwa wachezaji Yanga, pongezi kwa kocha Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Mar 2018
Pongezi kwa wachezaji Yanga, pongezi kwa kocha Lwandamina
Yanga jana imeonyesha inaweza kupambana katika mazingira ya aina yoyote. Matokeo ya mchezo ya kwanza ndio yaliyoiondosha Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.

Kocha George Lwandamina na wachezaji wote wanastahili pongezi nyingi kwa juhudi kubwa waliyoonyesha nchini Botswana jana.

Katika mchezo wa jana Yanga iliweza kurekebisha kikamilifu makosa waliyofanya jijini Dar es salaam kwenye mchezo wa kwanza.

Hawakuwapa kabisa Township Rollers nafasi ya kukaa na mpira kwa muda mrefu na hivyo kuwapa wakati mgumu kwa muda wote wa mchezo.

Rollers walilazimika kupiga mashuti ya mbali baada ya kushindwa kuipenya ngome ngumu ya Yanga iliyokuwa chini Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Said Juma bila kumsahamu mlinda lango Youthe Rostand ambaye sasa amekuwa 'mtamu'.

Yanga kama ingecheza vile kwenye mchezo wa kwanza, hawa Township Rollers walikuwa wanaondoka.

Pengine tatizo la majeruhi ndilo lililovuruga mipango ya kocha Lwandamina kwenye mchezo wa kwanza.

Hata hivyo Yanga ikiwa ni timu pekee kutoka Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Kimataifa ina nafasi ya kutinga hatua ya makundi katika michuano ya kombe la Shirikisho.

Benchi la ufundi na wachezaji wanatambua umuhimu wa kutumia vyema uwanja wa nyumbani. Kama Yanga itaibuka na ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani, inayo nafasi kubwa ya kutinga hatua hiyo.

Mchezo dhidi ya Township Rollers umedhihirisha ni jinsi gani Yanga ilivyoimarika katika kujilinda inapokuwa inacheza ugenini, kinachohitajika ni matokeo ya nyumbani tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’