FT : Township Rollers 0-0 Yanga, agg(2-1)

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Mar 2018
FT : Township Rollers 0-0 Yanga, agg(2-1)
Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na mabingwa wa Botswana, Township Rollers kwenye mchezo wa pili uliozikutanisha timu hizo leo.

Towsnhip Rollers imetinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam March 07.

Safu ya ulinzi ya Yanga pamoja na mlinda lango Youthe Rostand walilikuwa imara leo licha ya mashambulizi mfululizo kutoka kwa vijana wa Roller, hawakuruhusu bao kutinga nyavuni kwao.

Yanga sasa inasubiri kupangiwa moja ya timu zitakazotinga hatua ya 16 bora michuano ya kombe la Shirikisho kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Licha ya kutopata ushindi leo, kikosi cha Yanga kinastahili pongezi kwani kimecheza vizuri hasa katika kujilinda licha ya changamoto ya maamuzi yasiyoridhisha kutoka kwa mwamuzi wa mchezo huo ambapo wachezaji takribani sita wa Yanga walionyeshwa kadi za njano.

Baada ya kukosa kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa, Yanga sasa inahitaji kujipanga ili kuhakikisha inatinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’