Afisa Habari wa Yanga Ali kamwe amesema mchezaji Gael Bigirimana sio mchezaji wa Yanga bali aliomba kufanya mazoezi na kikosi wakati huu wa pre-season kuelekea msimu ujao
Kuonekana kwa Bigirimana katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea Avic Town kuliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya watu wakizusha kuwa mchezaji huyo ni sehemu ya kikosi cha Yanga
"Wanachopaswa kujua mashabiki na wanachama wa Yanga ni kwamba Gael Bigirmana kwa sasa sio mchezaji wetu, kuonekana Avic Town na wachezaji wetu ni kawaida kwa wachezaji kurejea kwenye vilabu walivyowahi kuvitumikia kwa Furaha na Amani"
"Gael aliomba kuja kufanya mazoezi na waliokuwa waajiri wake, amerejea kama rafiki ili kujiweka sawa kwakuwa bado ni mchezaji na anajiandaa kwa kuwa ana mipango yake na vilabu Vingine"
"Tuliona hata Khalid Aucho na Aziz Ki wakati wako mapumziko walirejea kwenye vilabu walivyotokea na kuendelea kufanya nao mazoezi na msimu unapoanza basi wanarejea kwenye majukumu yao," alisema Kamwe