Klabu ya Kaizer Chiefs imemshukuru Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi kwa mwaliko wa kushiriki tukio kubwa la Wiki ya Mwananchi lililofanyika Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Aidha Kaizer imeshukuru kwa kupewa mwaliko wa kutembelea visiwa vya Zanzibar ambako walipata nafasi ya kuonana na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na Mama Fatma Karume
"Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said, kwa kutoa mwaliko wiki iliyopita pia kukutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na Mama Fatma Karume, mama wa Taifa, kwani alikuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Aman Karume"
"Amakhosi pia inapenda kutoa shukurani zetu kwa mashabiki wa Young Africans SC waliotushangilia wakati wa mechi yetu. Shauku yao iliongeza msisimko kwa tukio zima, na kulifanya tukio lisilosahaulika kwa kila mtu aliyehusika"
Thank you Yanga!
— Kaizer Chiefs (@KaizerChiefs) July 28, 2023
We want to extend a special thank you to The President of Young Africans SC Hersi Ally Said, for extending the invitation last week to meet the President of the Revolutionary Government of Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi and Mama Fatma Karume, the mother of our⦠pic.twitter.com/ydu8U7jqF5