Anayetajwa kuwa mbadala wa Djuma Shabani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2023
Anayetajwa kuwa mbadala wa Djuma Shabani

Yanga inatajwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia wa Asec Mimosas Yao Kouassi Attohoula (26)

Kwa walioifuatilia Asec Mimosas katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu uliopita, lazima wamfahamu huyu mwamba

Mahiri katika ulinzi na hatari katika kusukuma mashambulizi kwa timu pinzani. Anavyocheza beki namba 2 unaweza kudhani ni winga lakini pia anamudu kucheza nafasi hiyo

Alikuwa miongoni mwa silaha muhimu zilizoisaidia Asec Mimosas kucheza nusu fainali ya kombe la Shirikisho ambapo walitolewa na USM Alger ambao waliibuka mabingwa kwa ushindi wa bao la ugenini dhidi ya Yanga

Yao yalikuwa mapendekezo ya kocha aliyeondoka Yanga, Nasreddine Nabi ambaye aliweka bayana kutoridhishwa na kiwango cha Djuma Shabani 'Soldier ya Bemba' ambaye mechi nyingi za mwishoni mwa msimu uliopita alimpisha Dickson Job katika nafasi yake

Kumekuwa na taarifa kuwa Djuma anawindwa na klabu ya TP Mazembe, ni wazi kama Yanga itamsajili Yao, huo utakuwa mwisho wa Djuma na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’