Baada ya utambulisho wa beki kisiki Gift Fred aliyetua Yanga kutoka SC Villa ya Uganda, Wananchi watashusha silaha nyingine. Imeelezwa leo mtikisiko utakuwa mkubwa zaidi pengine kuliko jana
Mpaka sasa Yanga imetambulisha wachezaji wawili, Nickson Kibabage na Gift, bado kuna kuna silaha nyingine zinasubiri kuwekwa hadharani
Je kiungo Jonas Mkude amesajiliwa na Yanga? Vipi yule winga kiberenge Max Mpia Nzegeli kutoka DR Congo? Na namba sita je, ambaye Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amemtaja kama kiungo mahiri zaidi Yanga kuwahi kumsajili na kucheza ligi ya Tanzania Bara?
Hii ni wiki ambayo Mwananchi hupaswi kukosa bando katika simu yako, kwani majibu ya maswali hayo yote yatapatikana
ADVERTISE HERE