Habari hasi kuhusu Yanga zimetawala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hii ni ishara kwa kiasi gani Yanga imefanikiwa na sasa wapinzani wake wanajaribu kutumia mbinu za 'cuba' kujaribu kuvuruga utulivu
Mara utasikia kuna wachezaji wameandika barua wanataka kuondoka, mara kocha hawataki wachezaji fulani, mara sijui Mayele kafanya nini, mara Yanga wamefungiwa kusajili mara GSM anataka kuondoka...! Hizi ndio habari ambazo Mwananchi utakutana nazo katika mitandao ya kijamii na hata baadhi ya magazeti
Hata wale waandishi wa Habari Waandamizi ambao wamejijengea imani na kufuatiliwa sana, wamekubali kutumika kusukuma ajenda hizi zenye lengo ovu
Leo Wananchi wameamka na taarifa ya Mtendaji wao Mkuu Andre Mtine kuondoka! Ikiripotiwa na Wanahabari ambao watu wanawaamini sana
Inasikitisha kwa sababu hata Mtine mwenyewe ambaye anatarajiwa kurejea nchini leo akitokea Zambia alikokuwa likizo, ameshangazwa na taarifa hizo
Jambo la msingi kwa shabiki na Mwanachama wa Yanga usiamini kila unalokutana nalo huko mitandaoni na kwenye baadhi ya magazeti kwani asilimia 90 ni porojo tu
Nafikiri huu ni wakati ambao Wananchi wanapaswa kuwa wamoja ili kuhakikisha wale wenye nia ovu ya kuvuruga wanashindwa