Mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kujivunia mafanikio ambayo timu yao ilipata katika michuano ya vilabu barani Afrika msimu uliopita
Kucheza fainali ya kombe la Shirikisho na kufanikiwa kukusanya alama 20 katika msimu mmoja haya ni mafanikio makubwa
Kwa mara ya kwanza Yanga imeingia katika orodha ya klabu 20 bora barani Afrika
Katika orodha iliyotolewa na CAF, Yanga inashika nafasi ya 16 ikiwa imepanda kwa nafasi 59 kutoka nafasi ya 75 msimu uliopita
Yanga imezipita timu kama Al Hilal inayoshika nafasi ya 19, Orlando Pirates (17), Asec (18), Kaize CHiefs (24), El Marreikh (25), AS Vita (26) na nyinginezo nyingi
Wakati wale wa upande wa pili wakitamba kushika nafasi ya saba kwa alama walizokusanya kwa miaka mitano, Wananchi wamehitaji msimu mmoja kupanda mpaka nafasi ya 16
Jambo la uhakika kama Yanga itafanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwenye msimu ujao, itaingia katika orodha ya klabu 10 bora, yatakuwa mafanikio makubwa kufikiwa katika misimu miwili tu
Ni suala la muda tu Yanga 'itafyeka' hiki kichaka cha ubora CAF ambacho ndicho kilichobaki..!