Yanga kuamua hatma ya Mayele

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jul 2023
Yanga kuamua hatma ya Mayele

Kabla ya Yanga kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya (2023/24) hatma ya mshambuliaji Fiston Mayele itakuwa imefahamika

Mayele anatarajiwa kufanya kikao cha mwisho na viongozi wa Yanga siku ya Jumatatu ambapo baada ya kikao hicho itafahamika kama anabaki au anauzwa

Yanga ilimuwekea Mayele ofa ya kuongeza mkataba lakini wakati huohuo zipo ofa nono kutoka klabu nyingine jambo linalomfanya mchezaji huyo adai maslahi zaidi

Mayele amethibitisha kuwa watafanya kikao cha mwisho na uongozi siku ya Jumatatu, siku ambayo wachezaji wote wametakiwa kuripoti Avic Town

"Ni kweli zipo ofa kutoka hapa Afrika, Ulaya nchi ya Ubelgiji na Qatar, uongozi wa Yanga unafahamu. Mimi bado ni mchezaji wa Yanga mpaka 2024, Tutakaa na uongozi kikao cha mwisho, Jumatatu tutajua kama nitaondoka au nitabaki Yanga," alisema Mayele

Presha imekuwa kubwa kwa Mayele ambaye kwenye moja ya mahojiano yake alibainisha wazi anachohitaji ni fedha taarifa za ndani zikidokeza kuwa hajakubaliana na ofa ya mshahara ambao Yanga wamemuwekea mezani (Takribani Milioni 34 kwa mwezi)

Mshahara huo ungemfanya Mayele kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania lakini ni wazi ofa zilizopo mezani ni nono zaidi

Huenda Yanga ikalazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kumuuza na kurudi sokoni kusaka mshambuliaji mbadala 

Kwani kama hatasaini mkataba mpya, ataondoka bure mwishoni mwa msimu ujao mkataba wake utakapomalizika

kesi yake inafanana na kesi ya mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo huku akigomea kuongeza mkataba

PSG wamempa Mbappe mpaka Julai 31 awe ameamua, kusaini mkataba mpya au kuuzwa kwani klabu haiko tayari aondoke bure

Yanga ndio iliyokuza 'brand' ya Mayele akipata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ya DR Congo kwa mara ya kwanza na sasa kugombewa na klabu nyingi

Yanga haiwezi kukubali mchezaji huyo aondoke bure msimu ujao kama haiwezekani kuongeza mkataba basi wanaweza kuchukua fedha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’