Yanga haijakurupuka kumleta Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jun 2023
Yanga haijakurupuka kumleta Gamondi

Uongozi wa Yanga haukukurupuka kumuajiri Kocha Miguel Gamondi kurithi mikoba iliyoachwa na Profesa Nasreddine Nabi ambaye huenda akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs katika saa 48 zijazo

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefichua kwa nini Yanga iliamua kumuajiri Gamondi na kuachana na makocha wengine baadhi yao wakiwa na majina makubwa ambao waliomba kuinoa Yanga

Kamwe amebainisha kuwa Yanga ilianza mawasiliano na Gamondi baada ya mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe iliyopigwa DR Congo

"Timu yetu imekuwa na mafanikio makubwa katika misimu miwili iliyopita chini ya Kocha Nasreddine Nabi, hivyo tulipaswa kutafuta kocha ambaye ataendeleza hapa alipoishia Nabi"

"Nabi alitengeneza muundo wa timu yenye tabia fulani ya uchezaji, tulipaswa kupata kocha ambaye ataendeleza utamaduni huo na sio kocha ambaye ataleta mifumo mipya katika timu angeweza kutuvuruga"

"Tunaamini Gamondi ni mtu sahihi kwa sababu mbinu na mifumo yake inashabihiana kabisa na vile ambavyo timu yetu imekuwa ikicheza chini ya Nabi. Uzuri ni kwamba tumekuwa na mawasiliano nae muda mrefu kabla ligi haijamalizika, amepata muda wa kufuatilia baadhi ya mechi tulizocheza"

"Ni kocha ambaye mpaka sasa anafahamu mahitaji ya timu yetu na hata katika maboresho ambayo tumefanya, Gamondi ameshiriki kwa asilimia 100%," alisema Kamwe

Ujio wa Gamondi unakwenda kukoleza upinzani wa jadi uliopo kati ya Yanga na Simba upande wa benchi la ufundi

Kocha wa Yanga Gamond ni raia wa Argentina na Robertinho wa Simba ni raia wa Brazil, nchi zao zina upinzani wa jadi katika soka

Mchambuzi wa soka Azam TV Ramadhan Mbwaduke amemtaja Gamondi kuwa anakwenda kuifanya Yanga iwe hatari zaidi pengine kuliko wakati wa Nabi

"Mimi naweza kusema Gamondi ni Nabi aliyechangamka kwa sababu yeye hupendelea soka la pasi lakini za kwenda mbele (direct footballl)"

"Mashabiki wa Yanga watarajie timu yao itaendeleza utamaduni wa pasi nyingi lakini wakati huu zitakuwa zenye lengo la kulifikia haraka lango la wapinzani," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’