Kocha wa Asec apenya usaili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2023
Kocha wa Asec apenya usaili Yanga

Kocha Mkuu wa Asec Mimosas Julien Chevalier anapewa nafasi ya kurithi mikoba ya Nasreddine Nabi katika kikosi cha Yanga

Chevalier anaweza kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kumrithi Nabi kutokana na makocha hao kushabihiana aina ya soka wanalofundisha

Katika misimu miwili akiwa na Asec Mimosas, Chevalier ametwaa Ligi Kuu ya Ivory Coast mara mbili huku akiisaidia Asec kufika hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika 2021/22

Msimu uliomalizika aliisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya Shirikisho ikitolewa na USM Alger ambao ndio mabingwa wakibebwa na kanuni kuishinda Yanga

Kocha huyo raia wa Ufaransa ni muumini soka la pasi fupi fupi (tiki-taka), mkataba wake na Asec unamalizika mwishoni mwa mwezi huu, Juni 30

Huyu ndiye kocha aliyemfanya Stephane Aziz Ki kuwa staa pale Asec kabla ya Yanga kumuona na kumsajili msimu uliopita

Yanga inatarajiwa kumtangaza kocha mkuu kabla ya mwezi huu kumalizika, ataanza majukumu yake mwanzoni mwa mwezi ujao wakati wa pre-season

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’