Yanga haitafanya usajili mkubwa - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2023
Yanga haitafanya usajili mkubwa - Hersi

Juzi baada ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azma (ASFC) dhidi ya Azam Fc ambao Yanga iliibuka mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Mkwakwani, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliweka bayana maboresho ambayo mabingwa hao wa nchi watafanya kuelekea msimu ujao

Hersi alisema kushinda mataji yote ya ndani kwa misimu miwili mfululizo halikuwa jambo rahisi, ili kuendelea kufanya vizuri msimu ujao watafanya maboresho katika maeneo machache ambayo yameainishwa katika ripoti ya benchi la ufundi

"Pamoja na mafanikio haya, lazima tuboreshe baadhi ya maeneo ili tuendelee kuwa washindani. Haimaanishi wachezaji hawa tulionao hatuwaamini la hasha! Ila yako maeneo ambayo tunadhani tunahitaji kuboresha ili tufanikiwe zaidi ya vile tulivyofanya msimu huu hasa kwenye michuano ya CAF," alisema Hersi

Tayari Yanga inahusishwa na nyota kadhaa ambapo mpaka sasa inaaminika Yanga tayari imekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji

Winga wa TP Mazembe Felippe Kinzumbi na kiungo aliyevunja mkataba na Al Hilal ya Sudan Fabrice Ngoma wanaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao

Katika safu ya ushambuliaji pia Yanga inahusishwa na Ranga Chivaviro ambaye ameachana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini baada ya timu hiyo kushuka daraja

Ni ahadi ya Injinia Hersi kusajili mchezaji kutoka Ligi Kuu ya Afrika. Ahadi hiyo aliitoa katika moja ya mahojiano yake wakati yuko Afrika Kusini na Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’