Ni fainali CAF CC, mechi ya kihistoria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2023
Ni fainali CAF CC, mechi ya kihistoria

Jioni ya leo macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuwashuhudia Wananchi wakicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger

Ni mchezo wa mkondo wa kwanza ambao utapigwa saa 10 jioni wakati fainali ya pili itapigwa Algeria Ijumaa ijayo

Ni mechi ya kihistoria kwa Yanga na Tanzania kwa sababu hii ni mara ya kwanza mechi ya fainali ya michuano ya CAF inapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mwaka 1993 Simba walicheza fainali ya kombe la Washindi (Mashoud Abiola Cup)  mchezo dhidi ya Stella Abidjan ukipigwa uwanja wa Uhuru (Shamba la Bibi) hivyo leo historia itaandikwa dimba la Mkapa kwa mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) kupigwa katika uwanja huo

Nafasi nadra kwa mashabiki kushuhudia mtanange huo wa kihistoria, ni wazi siti zote 60,000 zitakuwa na watu kwani tiketi zote za mchezo huo zimeuzwa

Yanga inawania taji kubwa la kwanza barani Afrika, leo inahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kazi ugenini kwenye mchezo wa pili

Yanga imepata maandalizi mazuri, kocha Nasreddine Nabi, wachezaji wamezungumza jinsi walivyo tayari kwa mchezo huo

Sapoti ya mashabiki hakuna shaka itakuwa kubwa lakini muhimu Wananchi wanapaswa kushangilia kwa muda wote wa mchezo ili kuhakikisha morali ya wachezaji wao haishuki

Wachezaji wa Yanga wanahitaji kufunga bao mapema ili kuvuruga mbinu za wapinzani wao ambao inafahamika mbinu watakayotumia zaidi leo ni kucheza kwa tahadhari pamoja na kupoteza muda

Mipira ya adhabu na kona inapaswa kudhibitiwa vyema kwani hiyo ndio itakuwa silaha kubwa ya USM Alger katika mchezo huo pamoja na kocha wao kudai hawakuja Tanzania kupaki basi

Hii ni siku ya kihistoria kwa Yanga na nchi kwa ujumla, matumaini ni kuona Yanga ikiibuka na ushindi mnono leo

Kila la kheri Yanga, kila la kheri Wananchi, Kila la kheri Mabingwa wa nchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’