Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Clement Mzize amesema ubingwa waliochukua jana unamaana kubwa katika historia ya maisha yake ya soka la ushindani
Mzize ambaye alitoa assist bao la pili la Yanga katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma Jiji, amesema mafanikio hayo yatamuongezea ari ya kuzidi kujituma ili aweze kufanya vizuri zaidi siku zijazo
"Namshukuru Kocha wangu Nasreddine Nabi kwangu ni kama baba kutokana na ushauri anaonipa lakini pia ni mtu mwenye imani kubwa na mimi hilo linanifanya kuongeza bidii na kujituma ili nimfurahishe," amesema Mzize.
Mshambuliaji huyo amesema kwa nafasi aliyopewa ataendelea kupambana ili msimu unaokuja aweze kufanya vizuri zaidi ikiwemo kuwa tegemezi kwenye kikosi cha kwanza.
ADVERTISE HERE