Jangwani kupigwa rangi na Berger Paints

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2023
Jangwani kupigwa rangi na Berger Paints

Klabu ya Yanga imeingia mkataba na kampuni ya Berger inayotengeneza rangi za Robbialac ambayo imeingia ushirika na watakuwa na jukumu la kupaka rangi jengo la makao makuu ya klabu hiyo 'Jangwani'

Pia Robbialac itatoa punguzo za bidhaa zao kwa mashabiki wa Yanga wenye kati za Uanachama

"Katika kutekeleza ahadi ya Rais wa Yanga Eng Hersi Said ya kuboresha Miundombinu ya Klabu, leo tunaitangaza kampuni ya Berger inayotengeneza rangi za Robbialac kama mshirika wetu ambaye atafanya kazi ya kupaka rangi jengo letu hapa Makao Makuu ya Yanga, Jangwani"

"Pia ni fursa kwa mashabiki wa Yanga wenye kadi ya mwanachama au Shabiki wa Yanga watapata punguzo la bidhaa za Robbialac," alisema Mfikirwa

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Berger Salim Bharwan amesema wanafurahi kufanya kazi na Yanga inayofanya vizuri ndani na nje ya nchi

"Tunaamini Yanga imekuwa ikifanya vizuri ndani na nje ya nchi, tunayo furaha kufanya kazi nao sisi kama kampuni ya Berger paints na tunayofuraha kuzindua kampeni yetu iitwayo MWAGA RANGI UIPENDAYO, na kipekee kabisa tunayo Slogan nyingine ya MWAGA RANGI NA YANGA," alisema Bharwan

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’