Yanga yaja na mkakati wa kushinda Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 Mar 2018
Yanga yaja na mkakati wa kushinda Botswana
Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar leo, kikosi cha Yanga kitaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Twonship Rollers.

Benchi la Ufundi linaloongozwa na kocha George Lwandamina linaamini Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri ugenini nchini Botswana kama itajiandaa kikamilifu.

Aidha uongozi wa Yanga umeandaa mpango mkakati wa kuhakikisha Yanga inaweza kupata matokeo nchini Botswana na hatimaye iweze kutinga hatua ya makundi ya michuano.

Moja ya mkakati ni kuhamasisha zaidi wachezaji kupambana ili kupata matokeo yatayowavusha hatua inayofuata.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema wakifanikiwa kufuzu makundi, sehemu ya fedha watakazolipwa zitakuwa zawadi kwa wachezaji.

“Litakuwa ni jambo la ajabu mtu ukapata fedha kama hizo halafu ukashindwa kuwapatia wale waliochangia kufanikisha hilo. Hivyo, uongozi tumepanga kufanya hivyo,” alisema.

“Hata hivyo, hatuwezi kutangaza ni kiasi gani hasa ambacho tutawapatia katika fungu hilo ili tusije kuwavuruga wakapoteza utulivu kwa sababu suala la fedha ni nyeti. Kimsingi ijulikane wazi tu kwamba tukifuzu, basi wachezaji watanufaika"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →