Huu ni wakati wetu Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2023
Huu ni wakati wetu Wananchi

Nafasi kubwa ya Yanga kujiweka katika mazingira mazuri ya kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kucheza hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kwa kuibuka na ushindi mnono nyumbani dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni, hii ikionekana ni zamu yao kuweka rekodi

Tangu mashindano hayo yalipoanzishwa rasmi mwaka 2003 baada ya kuunganishwa kwa mashindano ya Kombe la CAF na Kombe la Washindi Afrika, hakuna timu yoyote ya Tanzania na Afrika Mashariki iliyowahi kutinga fainali yake na Yanga inasaka fursa hiyo ya kuandika historia ya kuwa ya kwanza

Ubora wa kikosi ilichonacho, mbinu za Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi pamoja na faida ya hamasa ambayo itapata mbele ya mashabiki wake watakaojitokeza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa leo, vitaongeza chachu kwa Yanga kupata ushindi muhimu nyumbani ili isiwe na mlima mrefu wa kupanda katika mechi ya marudiano ugenini itakayochezwa wiki moja baadaye.

Uthibitisho wa ubora wa kikosi cha Yanga unatokana na kuwa na kundi kubwa la wachezaji ambao wanaonekana kufanya vizuri katika idara zao kwa mujibu wa takwimu za mashindano hayo kuanzia hatua ya makundi hadi sasa

Yanga ina wachezaji ambao wameingia katika tatu bora katika chati za wafungaji bora, wachezaji bora, mashuti yaliyolenga lango, ukokotaji mpira na kutoruhusu mabao

Mchezo huo wa leo utachezeshwa na marefa kutoka Misri na mwamuzi wa kati atakuwa ni Mahmoud El Banna atakayesaidiwa na Ahmed Hossam Taha na Samy Halhal huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Mahmoud Nagi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’