Historia itaandikwa siku ya Jumatano katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini
Mtanange huu utakwenda kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10 jioni
Ni historia kwa sababu katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, hakuna timu kutoka Tanzania imewahi kutinga nusu fainali ya mashindano ya CAF
Ndio maana kwa mashabiki wa soka nchini hasa Wananchi hii ni mechi ambayo haupaswi kuiacha ipite bila ya kwenda uwanjani
Mechi kama hizi huwa hazitokei kila mwaka, yawezekana itapita tena miaka mingi kuishuhudia timu ya Tanzania ikifika hatua hii
Afrika nzima kuna mechi nne tu za nusu fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho
Kuna timu nane tu katika bara lote la Afrika zitashiriki mechi hizo za nusu fainali, Yanga ni miongoni mwa timu hizo
Habari njema ni kuwa mchezo utapigwa mapema tu, saa 10 hivyo ni uhakika zile changamoto zilizojitokeza katika mechi iliyopita dhidi ya Rivers United hazitakuwepo
Mwananchi una siku mbili tu za kuhakikisha umekamata tiketi yao ili kuwaongezea wachezaji hamasa katika mchezo ambao Yanga ni lazima ishinde ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali