Sakata la Feisal; TFF imelinda maslahi ya Mpira

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2023
Sakata la Feisal; TFF imelinda maslahi ya Mpira

Baada ya Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutupilia mbali maombi ya kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyetaka kuvunja mkataba wake na Yanga, hakuna tena nafasi ya Shauri hilo kusikilizwa katika ardhi ya Tanzania

Kama Feisal hajaridhika na maamuzi hayo, anapaswa kwenda CAS/FIFA ambako kimsingi atashindwa kwa kuwa rejea itabaki kuwa maamuzi ya Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji

Nafasi pekee ambayo Feisal anaweza kuitumia kuvunja mkataba wake ni kufika meza ya mazungumzo na klabu ya Yanga, alipaswa kufanya hivyo tangu siku ya kwanza badala ya kuvunja mkataba kupitia Instagram!

TFF imelinda maslahi ya mpira wa miguu kwani alichofanya Feisal kama kingeidhishwa basi wachezaji wengi wangetumia utaratibu huo kuachana na klabu zao

Wachezaji na klabu zinapaswa kuheshimu mikataba, lazima utaratibu ufuate pale upande mmoja unapotaka kuvunja mkataba

Mkataba ambao hauna kasoro hauwezi kuvunjwa na upande mmoja, lazima pande zote mbili zikae na kufikia makubaliano

Njia pekee ya kumsaidia Feisal ni kumshauri afuate utaratibu kama ulivyoainishwa kama anataka kuondoka, Yanga haijamlazimisha Feisal, bali imelinda maslahi yake

Kama kuna timu inataka kumsajili Feisal inapaswa kupeleka ofa Jangwani, kama ni yeye mwenyewe anataka kuondoka kwa utashi wake pia anapaswa kwenda kuzungumza na waajiri wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’