Nabi ameahidi burudani na ushindi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2023
Nabi ameahidi burudani na ushindi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumapili katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United

Timu yake ikiwa mbele kwa mabao 2-0 ukiwa ni ushindi uliopatikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Nabi amewahakikishia Wananchi watapata burudani kutoka kwa timu yao kwani hawaendi kusaka nusu fainali kwa kupaki basi

"Utakuwa mchezo mzuri ambao tutacheza kwa malengo, tukifahamu aina ya matokeo ambayo tunayahitaji ili tusonge mbele"

"hatutakaa nyuma kuzuia tu, bali tutaweka uwiano mzuri baina ya kushambulia na kuzuia. Hatuwezi kuweka hadharani kila kitu lakini tumejipanga kuwapa furaha mashabiki wetu kwa mchezo mzuri ambao utaambatana na ushindi," alisema Nabi

Katika hatua nyingine, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema ipo changamoto ya kununua tiketi kwa wale wanaonunua kupitia mitandao ya simu

Kamwe amesema ni vyema mashabiki wakawa na utamaduni wa kununua tiketi mapema ili kuepuka changamoto za aina hiyo

Kamwe amewataka mashabiki waliokumbwa na changamoto hiyo kutembelea vituo vilivyotangazwa kununua tiketi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’