Bado hatujafuzu nusu fainali - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2023
Bado hatujafuzu nusu fainali - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohamed Nabi amesema bado hawajafuzu nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CAF kwani mchezo wao dhidi ya Rivers United haujamalizika, bado kuna dakika nyingine 90 kwenye dimba la Mkapa

Kauli hiyo ya Nabi imekuja wakati akihojiwa na vyombo vya habari nchini Nigeria baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho jana Jumapili, Aprili 23, 2023, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-0, katika Dimba la Godswill Akpabio, mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele dakika ya 73 na 81

"Sisi hatujaja hapa kujifurahisha, nazifahamu timu za Nigeria, kupata matokeo Nigeria ni vigumu sana, lakini tupo serious na mashindano haya. Siku zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu wajitahidi kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kuwaza matokeo ya uwanja wa nyumbani, ndicho hicho nilichokifanya"

"Rivers ni timu nzuri, mashindano ya Klabu Bingwa mwaka 2021/22, Rivers walituondoa katika hatua za awali, kulikuwa na sababu nyingi lakini zaidi timu yetu haikuwa kwenye ubora tulionao sasa hivi"

"Sisi Waafrika tunajuana, mechi hii haijaisha, bado kuna mechi nyingine ya marudiano Tanzania baada ya siku saba, kikao changu cha kwanza na wachezaji wangu itakuwa ni kuwasisitiza hilo. Nawaheshimu Rivers, kocha na wachezaji wao wote ni wazuri, lakini sisi tuna malengo ya kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya," alisema Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’