Tunawaheshimu Rivers United, tuko tayari - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2023
Tunawaheshimu Rivers United, tuko tayari - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United 

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Nabi alisema wanatambua wanakwenda kukabiliana na timu bora lakini malengo yao ni kupata ushindi

Nabi amesema hawataingia kwenye mchezo huo wakifikiri matokeo ya hatua ya makundi na kuwa lazima wawaheshimu wapinzani wao

"Hatujioni wakubwa kwa kuwa tumetoka kuongoza kundi. Tunawaheshimu wapinzani wetu kwani tunatambua ni timu nzuri lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunasonga mbele," alisema Nabi

"Tunakumbuka mwaka 2021 tulipoteza mechi dhidi ya Rivers United lakini ni kwa sababu hatukuwa tayari na pia zipo sababu nyingine kwa sasa tuko na timu tofauti na vilevile Rivers nao wamebadilika hivyo tunatarajia utakuwa mchezo mzuri wenye ushindani"

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, winga Bernard Morrison amesema Yanga haiko Nigeria kujifurahisha bali wamefuata ushindi

"Melengo yetu ni kuiwakilisha Yanga na Tanzania kwa ujumla. Hatuko hapa kwa sababu ya kujifurahisha bali tumekuja hata kufuata matokeo mazuri," alisema Morrison

Mchezo utapigwa kesho Jumapili saa 10 jioni (saa 8 Nigeria) katika uwanja wa Godswill Akpabio International

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’