Kamusoko kaikosa Township Rollers, sababu inaweza kuwa hii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2018
Kamusoko kaikosa Township Rollers, sababu inaweza kuwa hii
WanaYanga wameonesha mapenzi makubwa kwa kiungo wao fundi Thabani Kamusoko ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Mapema wiki hii uongozi wa Yanga ulithibitisha kuwa Kamusoko amepona. Na haikuwa kwa maneno tu, Kamusoko amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kimeweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers.

Amekuwa akifanya mazoezi kwa asilimia 100.

Ni busara za Mwalimu George Lwandamina kuamua asimtumie leo pengine ni kutokana na umuhimu wa mchezo wenyewe.

Mara nyingi mchezaji anayetoka kwenye majeruhi ya muda mrefu anahitaji muda wa kutosha ili kuhakikisha anarejea salama dimbani.

Ni kweli mashabiki 'tume mmiss' lakini lazima tukubali ni benchi la ufundi pekee linalofahamu hali yake ya kimchezo na atumike vipi.

Ilikuwa hivyo kwa Amissi Tambwe, baada ya kukosekana kwa muda mrefu, mashabiki waliweka presha kwa uongozi kuhoji nini mchezaji huyo hachezi licha ya kuelezwa amepona.

Leo hii Tambwe amerejea tena kitandani kuuguza majeraha yaleyale. Pengine aliihitaji muda zaidi kuimarisha afya yake ya ki-mchezo kabla hajarejeshwa dimbani.

Jambo la muhimu hapa sio lazima kila mchezaji acheze, bali acheze mchezaji anayeweza kuisaidia timu kwa wakati huo.

Hatari ya kumuanzisha mchezaji aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu kwenye mchezo kama huu ni kupunguza nguvu ya kikosi kwani bila shaka hawezi kuwa 'fit' sawa na wenzie.

Presha ya mechi inaweza ikampelekea aumie tena kwa kuwa atajilazimisha kucheza kama wengine walio mchezoni kwa miezi mingi.

Ndio maana huko duniani mchezaji anayekaa nje kwa muda mrefu harejeshwi moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza. Mara nyingi wanapelekwa timu za vijana wakapate 'match fitness'.

Na hata akirejea kikosi cha kwanza hawezi kuchezeshwa kwenye mchezo muhimu ambao timu inahitaji matokeo.

Sana sana atawekwa katika orodha ya wachezaji wa akiba na huenda akaingia kama timu itapata matokeo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’