Kamusoko yuko sawa, Chirwa sawa, Ngoma bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2018
Kamusoko yuko sawa, Chirwa sawa, Ngoma bado
Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa leo Jumanne kuikabili Township Rollers kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Yanga itashuka uwanjani ikiwa na kikosi chake kamili baada ya wachezaji wake wengi waliokuwa majeruhi kurejea.

Macho na masikio ya WanaYanga wengi yamepelekwa kwa kiungo fundi Thabani Kamusoko ambaye imeelezwa sasa yuko timamu kiafya, uamuzi wa kucheza au kutocheza unabaki kwa kocha George Lwandamina.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, Kamusoko ana nafasi yake kwenye mchezo huo. Hata kama hataanza tangu mwanzo, lakini huenda akapewa dakika kadhaa na benchi la Ufundi.

Mshambuliaji Obrey Chirwa naye imeelezwa kuwa yuko kamili kuivaa Township Rollers. hakuna mwenye mashaka na Chirwa hasa anapokuwa fiti.

Chirwa ni aina ya washambuliaji ambao mabeki hawapendi kabisa kukutana nao dimbani. Ana pumzi, ana nguvu halafu anajua kuwalazimisha mabeki wafanye makosa.

Chirwa ametengeneza ushirikiano mzuri na washambuliaji wengine wa Yanga akina Ibrahim Ajib, Pius Buswita na Emanuel Martin.

Hata hivyo mshambuliaji Donald Ngoma licha ya kuanza mazoezi hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Township Rollers.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema Ngoma bado anaendelea na program maalumu ya Daktari sambamba na beki Abdallah Shaibu 'Ninja'.

Habari njema ni kwamba Ngoma ana 'mzuka' wa kutaka kurejea dimbani haraka iwezekanavyo, Kukosekana mchezo wa kesho kunampa nafasi ya kujiimarisha zaidi kiafya kabla ya kurejea.

Yanga inashiriki michuano mitatu,ambayo ni FA, VPL na Ligi ya mabingwa hivyo inamuhitaji kila mchezaji ili kufanikiwa kufanya vizuri katika michuano yote.

Lakini kwa sasa nguvu zote zimeelekezwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwani baada ya dakika 180 Yanga inaweza kuoga 'mapesa' ya CAF kama itafuzu hatua ya makundi.

Kwa kutinga tu hatua ya makundi, pesa watakazolipwa na CAF ni sawa na kutwaa mataji 14 ya ligi kuu ya Vodacom!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’