Baada ya kutua Lubumbashi usiku wa kuamkia leo kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe, kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi yake ya kwanza
Mazoezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa TP Mazembe, yalishuhudiwa na Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohammed 'GSM'
Wachezaji 20 walishiriki mazoezi hayo, nyota wawili Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki wakitarajiwa kuungana na wenzao kesho Jumamosi
Meneja wa Yanga Walter Harrison alisema nyota hao wamechelewa kuungana na wenzao kutokana na majukumu yao katika timu za Taifa
Yanga itakamilisha mazoezi ya mwisho kesho Jumamosi tayari kwa mtanange huo ambao utapigwa Jumapili, saa 10 jioni
ADVERTISE HERE