Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Mchezo huo wa kuhitimisha hatua ya makundi, utapigwa April 02 kunako uwanja wa TP Mazembe huko Lubumbashi, DR Congo
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji walikuwa wakifanya mazoezi na kurejea makwao lakini leo wanaingia rasmi kambini Avic Town
Yanga itaondoka nchini Alhamisi March 30 ambapo wachezaji ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa wataungana na wenzao kabla ya safari huku baadhi yao wakiungana na timu hukohuko DR Congo
Yanga imejipanga kushinda mchezo dhidi ya TP Mazembe ili kuhakikisha inasalia kileleni mwa kundi D
ADVERTISE HERE