Twendeni DR Congo tukaisapoti timu yetu - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2023
Twendeni DR Congo tukaisapoti timu yetu - Injinia Hersi

Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amewataka wanachama na mashabiki kuchangamkia fursa ya kusafiri DR Congo kuiunga mkono timu yao katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa April 02

Hersi amesema Umoja mshikamano wa viongozi, sapoti ya wanachama na mashabiki umewezesha kufanikisha kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika huku wakiendelea kutimiza malengo ya ndani kwa kushinda Ngao ya Jamii, kuongoza ligi kwa tofauti ya alama nane pia wakitinga robo fainali kombe la Shirikisho la Azam

Hersi amesema wanahitaji Mshikamano na sapoti ya mashabiki kuhakikisha Yanga inashinda mchezo dhidi ya TP Mazembe ili kuongoza kundi D

"Dhamira yetu ilikuwa angalau kutinga hatua ya makundi lakini tumefanikiwa kuvuka na kutinga robo fainali"

"Klabu imeandaa utaratibu wa wanachama na mashabiki kwenda kushiriki mchezo dhidi ya TP Mazembe huko DR COngo ili kuongeza nguvu"

"Hii ni nafasi nzuri kwetu na kihistoria kuongoza kundi gumu katika mashindano ya Shirikisho. Faida kubwa ya kuwa kinara wa kundi ni kuwa; kwenye robo fainali tutapangwa na timu iliyomaliza nafasi ya pili katika kundi jingine na muhimu zaidi tutaanzia ugenini na kisha kumalizia mchezo wa pili nyumbani"

"Tunawaomba Wanachama na mashabiki wetu mchangamkie fursa hii mkawape nguvu wachezaji wetu," alisema Hersi

Jana Yanga ilitangaza nafasi kwa Wananchi kusafiri na kikosi cha Yanga kwenda DR Congo timu ikitarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam March 30. Gharama ya safari kwenda na kurudi ni Tsh 700,000/-

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’