Azam FC yaendeleza ubabe kwa Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2018
Azam FC yaendeleza ubabe kwa Singida United
Ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 20 imeendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti.

Moja ya michezo hiyo ni uliozikutanisha Azam FC dhidi ya Singida United miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kuzipa changamoto Simba na Yanga katika mbio za ubingwa.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi umemalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hii ni mara ya tatu kwa Azam FC kukutana na Singida United ambapo imeshinda mara mbili na kutoka sare mara moja.

Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe alama 38 lakini inabakia nafasi ya tatu nyuma ya Yanga yenye alama 40 na mchezo mmoja mkononi.

Mapema, Njombe Mji 'iliipapasa' Ruvu Shooting ya Masau Bwire kwa kuilaza mabao 2-1 huku mchezo kati ya Prisons dhidi ya Mbao FC ukivunjika kwenye dakika ya 50 baada ya mvua kubwa kuharibu mandhari ya dimba la Sokoine.

Mchezo huo ulivunjika wakati Prisons ikiongoza kwa bao 1-0 na utandelea dakika 40 zilizobaki kesho Jumapili asubuhi.

Kagera Sugar nayo imezinduka baada ya kuilaza Majimaji kwa mabao 2-1
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
19m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’