Matchday : Real Bamako vs Yanga, CAFCC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2023
Matchday : Real Bamako vs Yanga, CAFCC

Jioni ya leo majira ya saa 10 kwa saa za Mali (saa 1 usiku Tanzania) mabingwa wa Tanzania Yanga watashuka uwanja wa March 26 kuikabili Real Bamako katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ugenini ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo

Yanga iliweka kambi ya muda mfupi huko Mali kujiandaa na mchezo huo, wachezaji wakipata siku tatu za kufanya mazoezi na kuzoea hali ya hewa

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa vijana wake wako tayari kusaka matokeo mazuri katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu

Nae Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na Wanachama wa Yanga kuiombea dua timu yao iweze kuibuka na ushindi

Kamwe amesema wachezaji wote wako tayari walikamilisha mazoezi yao ya mwisho jana na hakuna mchezaji ambaye atakosa mchezo huo kwa sababu ya majeruhi

Mchezo huo utatanguliwa na mchezo wa mapema kundi D kati ya TP Mazembe dhidi ya US Monastir ambao unapigwa huko DR Congo

Kila la kheri Wananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’