Feisal anarubuniwa - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2023
Feisal anarubuniwa - Injinia Hersi

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema uongozi hauna tatizo na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' lakini wanasikitishwa na watu wanaomlaghai mchezaji huyo na kupelekea asiwe katika majukumu yake

Akihojiwa Clouds FM mapema leo, Hersi alisema kama kuna mtu anamlaghai Feisal anapaswa kupigwa vita na kila anyelitakia mema soka la Tanzania

Hersi amesema hamlaumu Feisal kwa kuwa anafahamu amewekwa katika mazingira magumu ambayo yalimfanya achukue maamuzi aliyochukua pasipo kuzingatia mkataba wake

"Kitendo cha mtu kumlaghai mchezaji kama kuna kitu kama hicho kimefanyika ni katika vitu vya hovyo vilivyowahi kutokea hapa nchini"

"Kuna taratibu zinaweza kufanyika na mchezaji akaenda kwenye Klabu nyingine lakini mtu anapita anamlaghai mchezaji hakuna binadamu anaweza kukwepa huo mtego"

"Simlaumu Feisal na kama kuna mtu wa hivyo anatakiwa apigwe vita huyo ni adui wa maendeleo ya mchezaji na Maendeleo ya mpira kwa ujumla"

"Mkataba ni ishu ya Taasisi haihusiani na ishu binafsi kama Rais au kiongozi yoyote mwingine. Matakwa ya kimkataba yanamuhitaji Feisal awepo kwenye klabu kwa hiyo Feisal ana mkataba anatakiwa arudi"

"Inapokuja ishu binafsi sisi kama viongozi ni wazazi pia hawa wachezaji mnaowaona kila siku pale sio kwamba hawatukosei. Wanatukosea kila siku lakini unawachukulia kama watoto na mzazi"

"Kile ambacho unahitaji kumuelekeza unakaa naye unamwelekeza, mnakwenda mbele. Feisal ni mchezaji wetu, Kijana wetu kuna watu wanaongeza chumvi huko kwenye mitandao. Hicho kwetu sio kitu muhimu. Tuna mkataba na Feisal hadi 2024. Ataendelea kuwa mchezaji wetu"

"Feisal akirudi tutampokea kwa mikono miwili. Tutamsapoti na ataendelea na majukumu yake," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’