FT : Yanga 3-1 TP Mazembe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2023
FT : Yanga 3-1 TP Mazembe

Kuna mwenye swali?, Hii ndio Yanga ya Wananchi sasa. Ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Wakiwa katika ubora wa hali ya juu, vijana wa Kocha Nasreddine Nabi walihitaji dakika 11 kufunga mabao mawili kupitia kwa Mudathir Yahya na Kennedy Musonda

Yanga ilitawala mchezo kwa muda mwingi kwenye kipindi cha kwanza huku TP Mazembe wakirejea wakiwa bora zaidi katika kipindi cha pili

Hata hivyo leo safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa bora sana chini ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto. Bao pekee la Mazembe lilifungwa na Alex Ngonga kupitia mpira wa adhabu

Wakati Mazembe wakitafuta bao la kusawazisha kwenye dakika za majeruhi, Tuisila Kisinda akamaliza shughuli ya leo akifunga bao mahiri baada ya pasi kutoka kwa Mayele

Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zinawapeleka mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D huku Wananchi leo wakiondoka na milioni 15 za Mama na milioni 3 za RC wa Mtwara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’