Morrison awaita Wananchi kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2023
Morrison awaita Wananchi kwa Mkapa

Winga wa Yanga Bernard Morrison amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe. Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 1 usiku

Pamoja na kutokuwa sehemu ya wachezaji watakaoshuka dimbani, Morrison amesema yuko bega kwa bega na timu katika maandalizi na matumaini yake ni makubwa leo watashinda mchezo

"Leo tuna mechi kubwa sana kwa hiyo twendeni tukutane uwanja wa Benjamin Mkapa. Wachezaji wetu wamejiandaa na wako tayari kutupa furaha siku ya leo. Jambo muhimu tunapaswa kwenda kwa wingi uwanjani kuwashangilia"

"Bahati mbaya mimi sitakuwa sehemu ya mchezo lakini niko bega kwa bega na wenzangu. Sapoti yenu ni muhimu sana leo," alisema Morrison

Morrison anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu

Amesema kwa sasa amepona kwa asilimia 85 hivyo anakaribia kuanza mazoezi

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’